Kocha wa Simba, Jackson Mayanja.
KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja amesema kuwa anakuja na sera mpya kwenye timu hiyo ya ushindi nje na ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Mganda huyo, tangu ametua kukinoa kikosi hicho hajapoteza mechi yoyote zaidi ya kutoa vipigo kwenye mechi tano mfululizo za ligi kuu nan moja ya Kombe la FA, sawa na pointi 18.
Kati ya michezo hiyo tano, mmoja wamecheza ugenini mkoani Shinyanga dhidi ya Kagera ambao waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililoifungwa na Ibrahim Ajib, akibakiza mechi nne; dhidi ya Stand, Mtibwa, Majimaji na Coastal Union.
Mayanja amesema anafahamu na ana uzoefu wa mechi za mikoani, hivyo amepanga kukiimarisha kikosi chake ili kuhakikisha haachi pointi mikoani.
Alisema hatabadilisha aina ya soka analolitumia- soka la pasi za haraka wakati timu yake ikiwa inamiliki mpira wakiwa wanalishambulia goli la wapinzani.
“Sitakuwa na mabadiliko yoyote ya aina ya soka ndani ya uwanja na badala yake nitaendelea kutumia mbinu na mfumo uleule ulionipa matokeo mazuri kwenye mechi zote za Uwanja wa Taifa Dar.
“Makocha wengi huwa wanabadili mifumo wanapocheza mikoani kutokana kwa kile wanachodai viwanja ni vibovu, kwangu sitabadili mfumo wala aina ya soka.
“Nina uzoefu mkubwa wa viwanja vya mikoani na badala yake nitaendelea na mfumo wangu uleule wa kupiga pasi za haraka wakati timu ikiwa na mpira tukiwa tunashambulia goli la timu pinzani, kikubwa ni kuhakikisha tunachukua ubingwa wa ligi kuu,” alisema Mayanja.
0 comments:
Post a Comment