Fahamu Ugonjwa Hatari wa ZIKA na Dalili Zake

Homa ya Zika ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi kijulikanacho kama “Zika Virus.” Na Ugonjwa huu unaenezwa na mbu aina ya Aedes ambaye huwa ana tabia ya kuuma asubuhi na pia nyakati za mchana/jioni. Aina hii ya kirusi ipo katika familia ya (Flavirus) ambapo pia vipo virusi vya ugonjwa wa dengue, Homa ya Manjano (Yellow Fever).

Mbu huyu anazaliana katika maji yaliyotuama hasa kwenye vyombo vya nyumbani, makinga maji ya paa za nyumba, matairi ya gari, ndoo, makopo nk.
Dalili zake
Dalili za ugonjwa huu zinafanana na za homa ya Dengue, ambazo ni homa, kuumwa na kichwa, maumivu ya viungo, macho kuwa mekundu na vilevile kupata vipele vidogo vidogo kama harara (Skin rashes).

Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia kati siku ya 2 hadi 7 tangu mtu alipoambukizwa kirusi cha homa ya Zika.
Wakati mwingine wagonjwa wanaweza kupata matatizo katika ubongo (Neurological Complications) na miguu kupooza (Gullein Barre Syndrome) na wajawazito huweza kujifungua watoto wenye ulemavu wa kichwa yaani kichwa kuwa kidogo kulingana na umri wa mtoto kitaalam Microcephaly.

Dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria. Hivyo basi, mtu anapojisikia homa ahakikishe anapima ili kugundua kama ana vimelea vya malaria au la.
Itaendelea toleo lijalo.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment