Thomas Ulimwengu.
Nicodemus Jonas, Dar es SalaamBAADA ya Mchezaji Bora wa Afrika, Mbwana Samatta kuondoka TP Mazembe na kusaini Genk ya Ubelgiji, ‘pacha’ wake, Thomas Ulimwengu ameweka wazi kuwa naye yupo njiani kuondoka Mazembe na jicho la kwanza limetua katika Klabu ya Saint Etienne ya Ufaransa.
Ingawa Samatta safari yake haijaiva kisawasawa kutokana na Mazembe kumuwekea kauzibe, bado ana asilimia 98 za kukipiga na mabingwa hao mara tatu wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Kumekuwepo na tetesi za Ulimwengu kutakiwa na Besiktas ya Uturuki, hata hivyo yeye ameibuka na kusema dili jingine lipo Ufaransa ambako amesema bado mchakato unaendelea.
Awali, meneja wake, Jamal Kisongo aliliambia gazeti hili kuwa kuna timu zipo nyingi zinazomhitaji Ulimwengu lakini kikwazo kikubwa ilikuwa ni safari ya Samatta kuondoka Mazembe ambayo ilikuwa na mchakato mzito sana kwani Wakongo hao hawakuwa tayari kumuachia.
0 comments:
Post a Comment