Hatimaye AZAM FC Wafungukia Kasi ya SIMBA SC

Said Ally, Dar es Salaam
KASI ya Simba kwa sasa wala haiwatishi Azam FC kwa kuwa wanaamini watawapiku tu.
Simba kwa sasa ipo sawa na Azam kwa pointi, lakini inashika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa nyuma ya Yanga kwa pointi moja, huku Azam ikiwa na michezo miwili mkononi.
Kocha msaidizi wa Azam, Denis Kitambi, ameliambia Championi Jumatano kuwa, kwa sasa wanakiandaa kikosi chao kushinda kila mchezo uliopo mbele yao kwa lengo la kuipiku Simba.


“Wametufikia kwa kuwa bado hatujacheza mechi zetu mbili, lakini baada ya kucheza hizo naamini hawatakuwa sawa na sisi. Tumepanga kushinda kila mchezo kwani nia yetu ni kuwa mabingwa msimu huu na wala si kushika nafasi ya pili.
“Tuna nafasi kubwa ya kuongoza ligi kwani kama tukishinda hizo mechi tutakuwa na pointi 48 na kuwaacha Simba kwa pointi sita huku Yanga tukiipita pointi tano,” alisema Kitambi.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment