AJIB Aingilia Vita ya TAMBWE, KIIZZA

Khadija Mngwai,na Said Ally
MSHAMBULIAJI wa Simba, Ibrahim Ajib amemtangazia vita straika wa Yanga, Amissi Tambwe, kwa kusema atahakikisha anamsaidia kwa nguvu zote Hamisi Kiiza kuhakikisha anaibuka kuwa mfungaji bora mwishoni mwa msimu.

Ajib ambaye amekuwa hatari kwenye michezo aliyocheza hivi karibuni kwa sasa ana mabao nane kwenye Ligi Kuu Bara huku akitengeneza nafasi nyingi sana kwenye timu hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ajib alisema kuwa, pacha yake na Kiiza imekaa vyema na atamsaidia kuhakikisha anafanikiwa kutwaa ufungaji bora mwishoni mwa msimu huu.
“Kombinesheni yangu na Kiiza ipo vizuri kwa kuwa tunaelewana na kwa upande wangu nimejipanga kumsaidia ipasavyo ili kuhakikisha anafunga katika kila mechi ili aweze kuwa mfungaji bora na ninaamini yeye ndiye atakayeibuka kidedea.
“Najua ushindani ni mkubwa kutokana na kila mchezaji kutaka kufunga na kusonga mbele zaidi lakini kwa kasi hii ya Simba tunahitaji mfungaji bora kutoka kwetu.
“Lengo letu ni kuhakikisha tunaisaidia timu yetu ipasavyo ili mwisho wa siku iweze kufanikiwa kutwaa ubingwa,” alisema Ajib.
Kwenye orodha ya wafungaji wa ligi kuu, Kiiza na Tambwe kila mmoja ana mabao 14 na hivyo Ajib anataka kumsaidia mwenzake kuwa mfungaji bora na kumbwaga Tambwe.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment