A-Kon
Wiki iliyopita msanii AY aliishia pale alipofanikiwa kuteuliwa katika kinyang’anyiro cha kushiriki Tuzo za Kora nchini Afrika Kusini akiwa ni Mtanzania wa kiume wa kwanza kuteuliwa katika tuzo hizo kupitia wimbo wake wa binadamu aliomshirikisha Mganda, Maurice Kirya.
Songa Nayo naye hapa…
Ambwene Yesaya ‘A-Y’
“Mpenzi msomaji wa makala haya ya MJUE AY nimeamua kusimulia maisha yangu halisi niliyopitia kutoka utotoni mpaka mahali nilipo kwa sasa kwa lengo moja tu la wewe kukufanya uamke ulikolala, usimame ulipokaa, uzungumze uliposhindwa kuzungumza na ujitume, uthubutu na kutumia fursa, fikiria kuhusu kipaji ambacho Mungu amekujalia, amekuzawadia, kitumie hicho ndicho kipato chako na pia mafanikio yako hivyo anza sasa.
“Basi tuzo zile za Kora sikufanikiwa kushinda lakini nilijisikia faraja na shujaa kuona nimeshiriki na hata kuona kumbe kazi ninayofanya inakubalika na mataifa mengi kwa hiyo nikaamua kukaza hasa katika muziki ili kufanya vizuri kwa kila wimbo.

“Mwaka 2006 niliteuliwa kushiriki tuzo nyingine zilizojulikana kama Kisima Music nchini Kenya kama Mwanamuziki Bora wa Kiume kutokaTanzania, mwaka uliofuata nilifanikiwa kushinda Tuzo ya Kilimanjaro Music ya Wimbo Bora wa Hip Hop (Best Hip Hop Single), nikapokea Tuzo ya Video Bora kutoka Tanzania katika Tuzo za Muziki za Kisima.
“Naweza kusema Mungu anapoamua kukuwezesha hakuna mwanadamu anayeweza kukushusha tena kwani Mwaka 2007 nilipata neema nyingine kwa kuteuliwa pia kugombea Tuzo za Lulu Afrika (Pearl of Afrika) katika kipengele cha Wimbo Bora wa Hip Hop.
“Mwaka 2008 nilipata tena Tuzo ya Kilimanjaro Music katika Kipengele cha Ushirikiano Bora (Best
Collaboration) pamoja na Tuzo ya Lulu Afrika Music katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume.
“Huwezi amini kati ya mwaka 2008-2009 msanii mkubwa wa kimataifa kutoka nchini Marekani ambaye ni mzaliwa wa nchini Senegal, Aliaume Damala (Akon) alizungumza waziwazi kuwa anavutiwa sana na staili ya uimbaji wangu na kunitabiria kuwa mmoja wa wasanii wakubwa wa siku zijazo kutoka Afrika ambaye ninaweza kufika kimataifa, Sikubweteka na sifa alizonipa Akon ila kawaida yangu ni kuzidi kukomaa, nikajitahidi kama kawaida mwaka 2010 tena nikateuliwa kuwania Tuzo ya Video Bora na Wimbo Bora wa Mahadhi ya Reggae kupitia Kilimanjaro Music (Kili).

“Baada ya hapo, mwaka 2010 nilifanikiwa kupokea Tuzo za Teen Xtra Music katika vipengele vya Video Bora, Wimbo Bora wa Mahadhi ya Reggae, Msanii Bora wa Mwaka, Kolabo Bora ya Afrika na nyingine nyingi. Pia ninayo tuzo kubwa inayotolewa nchini Ghana inayojulikana kama Museke ambapo nilichukuwa katika vipengele vya Wimbo Bora wa Mwaka Afrika Mashariki, Wimbo Bora wa Hip Hop pamoja na Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki.
“Naweza kusema mwaka 2010 nilipokea tuzo nyingi sana kwani baadaye niliteuliwa katika Tuzo za Kimataifa za Redio Ufaransa (International Radio France Awards).”
AY ni miongoni mwa wanamuziki wenye tuzo nyingi, unataka kujua nyingine? Tukutane wiki ijayo hapahapa.

0 comments:
Post a Comment