Magonjwa Hatari Yatokanayo na Kujamiiana- 4

TUNAENDELA kueleza tiba ya ugonjwa wa kisonono au gono tukianzia na ilipoishia wiki iliyopita:

Tulisema mgonjwa anaweza kutibiwa baada ya kuthibitika kuwa ana kisonono kwa dawa za jamii ya Penicillin kwa mfano Doxycyclin.

Mara nyingi kwa wagonjwa walio na umri wa chini ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa kuchomwa sindano.

Mgonjwa hutakiwa kufuata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizo kwani dawa nyingi huwa na madhara kwa wajawazito kwa mfano Doxycyclin.

Kwa kawaida ushauri hutolewa kwa washirika wote wawili walioambukizana gono, na ni vizuri wote wawili watibiwe hata kama mmoja wao hatakuwa na dalili za ugonjwa huu.

MADHARA YA GONO
Moja ya madhara anayoweza kupata mtu kutokana na ugonjwa wa gono au kisonono ni mwanamke kutoweza kuzaa yaani kuwa mgumba au mimba kutoweza kutunga.

agonjwa ya zinaa ya gono yana mchango katika kusababisha wanawake kutozaa kwani magonjwa hayo kwa asilimia 10 hadi 15 huweza kusababisha uvimbe katika Fupanyonga au Pelvic Inflammatory Disease (PID) na hasa kwa kuwa wanawake wengi wenye kisonono huwa hawaoneshi dalili.

Ugonjwa wa PID husababisha makovu katika mirija ya uzazi hali ambayo husababisha kushika mimba kuwa kugumu na matatizo wakati wa ujauzito. PID ni ugonjwa unaopaswa kutibiwa haraka.

Kwa upande wa wanaume ugonjwa wa kisonono huweza kuwafanya wasipate watoto kwani huwasababishia uvimbe katika sehemu ya mbele ya korodani ambako mbegu za kiume hutengenezwa.

Uvimbe huo usipotibiwa husababisha utasa.
Ugonjwa wa gono pia huweza kuathiri moyo, ubongo, ngozi na kadhalika kwa hivyo ni hatari kwa mtu yeyote na unahitaji kutibiwa mapema.

Pia ugonjwa huo huleta madhara au uvimbe kwenye maungio ya viungo, ambapo vimelea vinavyosababisha kisonono huweza kusambaa kwenye damu na kuleta maambukizo kwenye sehemu nyinginezo mwilini.

Maambukizo hayo huleta homa, vipele, vidonda kwenye ngozi, maumivu ya viungo na uvimbe.
Vilevile wanawake ambao ni wajawazito na wameambukizwa gono wako kwenye hatari ya mimba kutoka au kuzaa mapema kabla mimba haijatimiza umri wake (Preterm labor).
Mwisho.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment