Hamis KIIZA Amliza KERR wa SIMBA SC

kiiza-akishangilia-baada-ya-kutikisa-nyavu-uwanja-wa-taifa-dar-es-salaam_f9e7nzxc6j531t6oujg70lpkpMshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza.
Sweetbert Lukonge, Zanzibar
MICHUANO ya kuwania Kombe la Mapinduzi inafikia tamati Jumatano hii ambapo bingwa atapatikana.
Hata hiyo, mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza amemweka katika wakati mgumu kocha mkuu wa timu hiyo, Muingireza, Dylan Kerr ambaye amejikuta akitumia muda mwingi kulalamika.

Tangu kuanza kwa mashindano hayo, Kerr amekuwa hafurahishwi na kiwango cha Kiiza pamoja na washambuliaji wake wengine kutokana na kupoteza nafasi nyingi za wazi wanapokuwa uwanjani.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kerr alisema kuwa, hali hiyo inamfanya ajisikie vibaya kwani kila siku amekuwa akimpigia kelele mshambuliaji huyo raia wa Uganda pamoja na wenzake kuwa makini uwanjani na kuzitumia vizuri nafasi wanazopata lakini imekuwa ni kazi bure.
“Tunacheza vizuri sana lakini tatizo kubwa lipo katika umaliziaji kwani tumekuwa tukipoteza nafasi nyingi sana za kufunga.
“Nimekuwa nikiumia sana kila ninapoona hivyo, kwani matokeo ya bao moja tunayopata mara kwa mara, hayafurahishi ni kama vile tunashinda kwa bahati.
“Hakika Kiiza na wenzake wanapaswa kubadilika, wajitume zaidi na kuhakikisha wanazitumia vizuri nafasi wanazopata hata katika michuano ya Ligi Kuu Bara,” alisema Kerr.
Mpaka kufikia jana jioni kabla ya mechi ya nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi, Kiiza hakuwa na bao lolote.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment