Sweetbert Lukonge, Zanzibar
KILA lenye mwanzo lina mwisho wake, hivyo ndivyo unavyoweza kusema 
baada ya wachezaji wawili wa kimataifa wa Yanga, Wazimbabwe, Donald 
Ngoma na Thabani Kamusoko kutengwa klabuni hapo.
Hivi sasa wachezaji wao kila moja wao anapofunga bao, wamejikuta 
wakishangilia peke yao bila ya kupata sapoti ya wenzao. Wamekuwa 
wakishangilia kwa staili ya kushikana mabega huku wakiwa wameunganisha 
vichwa vyao na kuinama kidogo.
Siku za hivi karibuni staili hiyo ya ushangiliaji wa wachezaji hao 
ilizua gumzo jijini Dar es Salaam kutokana na kujadiliwa mara kwa mara 
katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Hata hivyo, visiwani hapa pia iliibua gumzo kwa mashabiki wa soka 
siku ambayo Ngoma aliiwezesha Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 
ilipocheza dhidi ya Mafunzo FC ambapo walishangilia kwa staili hiyo, 
hali iliyosababisha wachezaji hao kutengwa na wenzao.
“Hivi sasa kila wanapofunga sisi tunashangilia nao kama kawaida 
lakini ile staili ya kushikana mabega na kuunganisha vichwa huku tukiwa 
tumeinama tumewaachia wenyewe.
“Tumekuwa tukichafuliwa sana katika mitandao ya kijamii hivyo tumeona
 tuwaachie wao ila sisi tutakuwa tukishangilia nao kawaida mpaka hapo 
watakapokuwa wamepata staili nyingine,” alisema mchezaji huyo.
0 comments:
Post a Comment