Los Angeles, Marekani
MWANAMUZIKI wa Pop, Selena Gomez huenda ameshapata tulizo la
moyo wake baada ya kuonekana hadharani na rafiki wa karibu wa Justin
Bieber, Niall Horan wakipigana mabusu.
Kwa
mujibu wa jarida la US Weekly, juzi (Ijumaa) katika kusherehekea siku
ya kuzaliwa ya Jenna Dewan wawili hao walionekana kuingia kila mmoja kwa
wakati wake lakini walipokuwa ndani walikuwa karibu sana kiasi cha
kupigana mabusu bila wasiwasi.
Jarida hilo linafunguka zaidi kuwa si mara ya kwanza kwa wawili hao kuwa karibu kwani hivi karibuni wakiwa Los Angeles katika Tamasha la Jingle Ball walipanda jukwaani na kupafomu pamoja na imekuwa kawaida yao kutoka ‘out’ na kupata chakula cha usiku pamoja.

Mbali na hiyo, wawili hao pia walikuwa pamoja katika usiku wa tuzo zilizofanyika Los Angeles, Marekani. (AMA)
0 comments:
Post a Comment