Mwanadada Khloe Kardashian amenaswa
akiwasili katika hospitali ambayo dada yake, Kim Kardashian
amejifungulia mtoto wake wa pili jana asubuhi.
Khloe akiwasili hospitali na gari lake aina ya Bentley.
Khloe amenaswa leo na mtandao wa TMZ akiwasili katika Hospitali ya
Cedars-Sinai iliyopo Beverly Hills nchini Marekani akiwa katika gari
lake aina ya Bentley yenye rangi nyeupe tayari kwenda kumlaki mtoto.
Mwanamitindo na mtangazaji maarufu wa Kipindi cha Keeping Up With The
Kardashian, Kim Kardashian na mumewe ambaye ni staa wa muziki Kanye
West jana asubuhi walipata mtoto wao wa pili wa kiume.
0 comments:
Post a Comment