KUNDI
maarufu zaidi kwa sasa la hip hop nchini, Weusi limeweka wazi kumaliza
kufyatua kazi zake kwa mwaka huu baada ya kutoa ‘hit songs’ kadhaa wiki
chache zilizopita na kuwataka mashabiki wake kuwasubiri upya mwakani.
Hivi karibuni, kundi hilo kupitia memba wake, Nikki wa Pili, alitoa
Baba Swalehe na Joh Makini akaachia Don’t Bother aliomshirikisha AKA wa
Afrika Kusini, huku Original ya G Nako ikitarajiwa kuwa hewani muda
wowote kuanzia sasa.
Hata hivyo, Nikki ameliambia Championi Jumatano, kuwa kazi moja
iliyobaki ni ya Bonta pekee ambayo nayo ipo jikoni na itatoka kabla ya
mwaka huu kumalizika, hivyo kufunga hesabu za kazi za Kampuni ya Weusi
kwa mwaka huu. Wimbo huo wa Bonta unaitwa Usirudi Jela aliomshirikisha
Belle 9 na Nikki.
“Tunashukuru tumetambulisha kazi mbili hivi karibuni na zimeeleweka,
itatoka Original ya G Nako kisha itafuata ya Bonta ambayo ipo jikoni na
baada ya hapo itakuwa mwisho kwa mwaka huu mpaka mwakani, tunashukuru
mashabiki wetu kwa kuwa nasi na tunaamini tutaanza pamoja mwakani,”
alisema Nikki.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment