Habari wakuu,
Kumekua na tabia kwa baadhi ya wanawake ya kupenda waume zao na kuwachukia wazazi wa kike wa wawaume zao.
Hii tabia imekithiri katika baadhi ya ndoa nyingi, wanawake hao wamekua
wabinafsi sana, hawataki kuendeleza mahusiano ya mume wake na familia ya
mumewe.
Mfano, unakuta mtoto huyo wa kiume ni tegemeo la nyumbani kwao au wakati
mwingine sio tegemeo ila lazima atume kiasi flani cha matumizi nyumbani
kwao, lakini mkewe akiona hivyo anazuia hataki pesa zitumwe kwa mama
mkwe.
Wakati mwingine mama huyo anaumwa na anahitaji kuja kutibiwa kwa mwanae,
lakini mwanamke anakasirika na kumwambia mumewe asije kupata matibabu
nyumbani kwao.
Wanawake wengine wamekua wakigombana na mama wa waume zao bila hata
aibu, lakini eti akiwa na mumewe anampenda. Wanawake wenzangu tujifunze
kuwaheshimu mama wa waume zetu na tuwapende kama mama zetu.
Kama unampenda mumeo, mpende na mama mkwe
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment