KIM KARDASHIAN AMEJIFUNGUA MTOTO WA KIUME

STAA wa kipindi cha ‘keeping up with kardashian’ na mke wa rapa mahiri Kanye West,Kim Kardashian amefanikiwa kujifungua mtoto wa pili wa kiume hivi punde.

Taarifa rasmi katika ukurasa wake wa kijamii wa twitter inasema kuwa mama na mtoto wako salama huku wakingoja taratibu nyingine za kitabibu ili waweze kuruhusiwa nyumbani

Aidha baadhi ya mashabiki wa mwanamitindo huyo nguli Marekani,wamempongeza Kim kwa kufanikiwa kupata mtoto huyo ambaye ataungana na North kuleta furaha katika familia ya West

Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment