Said ally, Dar es Salaam
WASANII wa Yamoto Band wanatarajiwa kukinukisha nchini Marekani hivi karibuni kwa kufanya shoo tatu kali.
Mmoja wa waandaji wa shoo hizo, Dickson Mkama, ambaye pia ni mmiliki
wa Kampuni ya DMK Global Promotions alisema Yamoto watafanya shoo katika
maeneo matatu ikiwemo Kansas City, Washington DC na Houston Texas.
“Yamoto watakuwa na shoo Novemba 27, Kansas City, Desemba 5 watafanya
Washington DC na shoo ya tatu itakuwa Houston Texas ambapo wamejipanga
kuwarusha kikweli kweli mashabiki wao,” alisema DMK moja kwa moja kutoka
Marekani.
Band hiyo ambayo imejipatia umaarufu ndani na nje ya nchi na kutamba
na nyimbo zake kadhaa kama Cheza kwa Madoido, Niseme, Najuta na nyingine
kibao.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment