Mwanamuziki wa Nigeria, Wizkid.
MWIMBAJI wa Nigeria, Wizkid, amesema anaimba muziki si kwa kupata tuzo bali kwa kuwa anaupenda muziki kutoka moyoni.
Mwanamuziki huyo ambaye muziki wake unatamba duniani aliyasema hayo
katika mahojiano na jarida la International Magazine hivi karibuni.
Aliendelea kusema kwamba wimbo wake wa ‘Ojuelegba’ ambao baadaye alikuja
kumshirikisha rapa wa Marekani, Drake, hakufikiria kama ungekuja
kutingisha kiasi kile duniani.
“Nilijua ‘Ojuelegba’ ulikuwa wimbo mzuri, lakini sikuwahi kufikiri ungekuja kuwa maarufu kiasi kile.”
Akiwa ameanzia maisha yake eneo liitwalo Ojuelegba, ambako alizaliwa,
mwanamuziki huyo alitunga wimbo huo kuelezea jinsi watu wa huko
wanavyopigana na maisha ili ‘kutoka’ ambapo katika wimbo wake anasema
“wazazi wake bado wanaishi huko Ojuelegba” ambako wana nyumba.
0 comments:
Post a Comment