Wafahamu Mastaa Hawa wa TZ Ambao Tangu Watoke, Hawajachuja!

KATIKA maisha kuna kupanda na kushuka na ndivyo ambavyo binadamu tumeumbiwa, hii yote ni katika kujifunza zaidi.
Hapa nchini kuna wasanii wa fani mbalimbali ambao wamekuwa wakifanya vizuri wakati wote na wanaonekana kuwa na nyota za kung’ara zaidi kwani tangu wajiingize kwenye tasnia husika, hawajawahi kushuka, zaidi wanaendelea kupeta kukwea kilele cha mafanikio kila kukicha. Yaani ni mwendo wa mbele kwa mbele, nyuma mwiko!
Hapa Chini ni orodha ya baadhi ya mastaa hao ambao wameendelea kutesa.
diamond-platnumzDiamond.
Diamond
Nyota huyu kwa sasa unaweza kusema ndiye namba moja kwa ubora hapa nchini kutokana na mafaniko makubwa anayoendelea kuyazoa. Ana tuzo kibao za ndani na nje ya nchi. Jamaa tangu atoke na Ngoma ya Kamwambie mwaka 2009, anaendelea kulitingisha Bara la Afrika kwa kuzoa tuzo kila kukicha kimataifa zaidi. Kwa upepo ulivyo, Diamond siyo wa kushuka leo wala kesho.
wema-3Wema Sepetu.
Wema Sepetu
Mlimbwende asiyekaukiwa vituko ambaye nyota yake ilianza kung’ara mwaka 2006 baada ya kutwaa Taji la Miss Tanzania.
Baada ya hapo pia alifanikiwa kujikita kwenye uigizaji wa filamu kabla ya kujiingiza kwenye msululu wa wapenzi wengi mastaa aliowahi kutoka nao, kitu kilichomwongezea umaarufu na kuiteka nchi kwa kila jambo analotaka kulifanya bila kujali kama ni zuri au baya.
Farid Kubanda ‘Fid Q’
Mmoja kati ya wasanii wakali wa Hip Hop ambao wanafanya vizuri hapa nchini.
Fid Q amekuwa akitamba na vibao kadhaa vyenye mistari ya mafumbo na yenye mvuto kwa jamii lakini kazi yake imekuwa ikionekana kupendwa zaidi hapa nchini ila hajapata ‘exposure’ kivile nje ya nchi.
Pamoja na hayo, lakini ni miongoni mwa mastaa wenye heshima na wanaofanya vema kwani jina lake limebaki juu tangu alipoanza kufahamika mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Joh Makini
Alitoka kama masihara tangu mara ya kwanza aliposikika na ‘track’ yake ya Hao. Baadaye akawa gumzo na sasa anazidi kupasua kila kukicha, akivuka boda na kuzidi kuitangaza Hip Hop ya Tanzania.
Juhudi zake zinamfanya aendelee kufahamika zaidi kwenye ‘industry’ kwa kuzidi kujichanganya kwake na wasanii wa nje ya nchi.
Jux
Anatamba na Kibao cha Looking For You ambacho amekifanya na Joh Makini. Ukimuangalia tangu alipotoa ngoma yake iliyoibua gumzo zaidi ya Uzuri Wako mpaka leo bado jamaa ana-shine vilivyo.
Mistari yake ya kimahaba ambayo inawavuta watoto wazuri na vijana wa mjini inazidi kumfanya aendelee kusikilizwa siku hadi siku, ‘lifestyle’ yake na ‘mitupio’ pia inawavutia vijana wengi wa kileo kumfuatilia kwa ajili ya kufahamu mengi kupitia yeye.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment