NEW YORK, Marekani
HATARI! Staa wa Kibao cha Wiggle, Jason Derulo, ni kama
anajitafutia matatizo baada ya kuonekana akiwa kwenye mkao wa kimahaba
na Daphne Joy ambaye ni mzazi mwenzake na 50 Cent anayefahamika kwa
ukorofi.
Ripoti zinasema sasa ni rasmi Jason anatoka na ex wa 50 Cent ambaye
anafahamika kwa ukorofi kwenye mitandao ya kijamii, hivyo huenda
akamjibu Derulo, 26, baada ya kupata taarifa za uhusiano wao.
Ijumaa
iliyopita, Jason aliposti picha akiwa kwenye mkao wa kimahaba na Daphne
katika Mtandao wa Instagram huku Mtandao wa TMZ ukiandika kuwa hao ni
wapenzi rasmi na uhusiano wao ulianza wiki chake zilizopita baada ya
kukutana huko Uingereza.
Huu ni uhusiano wa kwanza kuwa wazi kwa Jason baada ya kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu, Jordin Sparks.
0 comments:
Post a Comment