Mdogo wa KIM KARDASHIAN, Kylie Achekelea Kuachana na TYGA

Modo Kylie Jenner.
Los Angeles, Marekani
MODO Kylie Jenner, 18, ameachana na mpenzi wake, Tyga, aliyedumu naye kwa miezi kadhaa, lakini mwishoni mwa wiki iliyopita alifanya bonge la sherehe kujipongeza kwa madai ya kutoka kifungoni.
Ishu ya kuachana kwa wapenzi hao illijulikana baada ya Kylie kutohudhuria bethidei ya Tyga, 26, wiki iliyopita.
Hata hivyo, mtandao mmoja wa kiburudani unadai chanzo cha kutemana kwa wapenzi hao walioanza uhusiano tangu Oktoba mwaka jana ni kutokana na Kylie kuona video ya Tyga ambaye aliwahi kuhusishwa kutoka na mrembo wa filamu za utupu, Mia Isabella, ‘akimchiti.’

Tyga.
Kylie alitumia Mtandao wa Kijamii wa Instagram kusema kuwa kamwe hatatoa machozi tena baada ya uhusiano wao kufika mwisho.
Mrembo huyo alituma kipande cha video kwenye Mtandao wa Snapchat akiimba Wimbo wa Been that Way wa Bryson Tiller unaozungumzia jamaa aliyetokea kumpenda mpenzi wake na kumpa kila kitu lakini ghafla alibadilika, hivyo naye kuamua kujiweka pembeni
Tangu ameachana na Tyga, Kylie sasa kampani yake kubwa ni ya mamodo wenzake tofauti na awali ambapo alikuwa akitumia muda mwingi kuwa na mpenzi wake huyo huku pia kwenye mitandao yake ya kijamii akisitisha kuweka meseji zenye ujumbe wa kimapenzi.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment