Na Dustan Shekidele, Risasi
MOROGORO: Kunani Kilosa? Mji wa
Kilosa mkoani hapa, kwa mara nyingine umekumbwa na majanga ya mafuriko
baada ya mvua kubwa kunyesha usiku ambapo safari hii yamesomba makaburi
yaliyopo katika Kata ya Magomeni.
Wananchi waliokumbwa na mkasa huo wakiwa wamejihifadhi kwenye jengo la shule.
Katika tukio hilo la hivi karibuni,
mwanahabari wetu alifika maeneo hayo na kushuhudia adha kubwa ya maji
yaliyojaa majumbani, majengo ya shule, zahanati na nyumba za kulala
wageni (gesti).
Zahanati ikiwa imezingilwa na maji.
Mashuhuda wanasema mvua hiyo
iliponyesha, baadhi ya watu walilazimika kutoka nje ya nyumba zao wakiwa
watupu. Baada ya kutokea kwa majanga hayo, baadhi ya kaya imebidi
zihifadhiwe kwenye majengo ya shule zilizopo eneo salama, lakini kilio
chao wakikielekeza kwenye makaburi hayo wakihofia kuwakosa moja kwa moja
wapendwa wao waliositiriwa hapo.
Wakihojiwa
na gazeti hili, baadhi ya waathirika wa tukio hilo baya, walieleza
kwamba chanzo cha mafuriko hayo kuvamia kata hiyo ya Magomeni ni tuta
kubwa lililopo eneo la darajani.
“Miaka yote sisi wakazi wa Magomeni, yanapofika majira ya masika huwa tunaishi roho juu.
Vyombo vikiwa nje baada ya nyumba zao kujaa maji.
“Miaka yote hali hii imekuwa
ikisababishwa na tuta kubwa darajani linaloelekeza maji hayo eneo hilo,”
alisema mmoja wa waathirika wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la
Asha Juma.
“Kinachouma
zaidi ni kusombwa kwa makaburi ya wapendwa wetu, ina maana tumepoteza
hata kumbukumbu ya makaburi yao,” alisema mwathirika mwingine.
Takriban
miaka mitatu iliyopita wananchi wa Kata ya Magomeni walivamiwa na
mafuriko yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa ambapo taarifa za awali za
viongozi wa Wilaya ya Kilosa zilidai kwamba katika mafuriko hayo ya
hivi karibuni hakuna aliyepoteza maisha.
Mbali
na mafuriko hayo, Wilaya ya Kilosa imekuwa ikikumbwa na majanga
mbalimbali yakiwemo ya ajali za mara kwa mara na mapigano ya wakulima na
wafugaji yasiyokoma.
0 comments:
Post a Comment