Waislam Nchini Walaani Mauaji ya Sheikh Bagir NIMR

IMG_20160112_165212 
Sheikh Hemed Jalala akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
2Baadhi ya waumini wakiwa kwenye dua maalum. 
WAUMINI na viongozi wa Chuo cha Kiislam cha Imam Swadiq kilichopo eneo la Kigogo Post, jijini Dar jana wamefanya dua maalumu ya kulaani vikali mauaji ya Waislamu nchini Saudi Arabia akiwemo mtetezi na mwanazuoni Ayatollah Sheikh Bagir Nimr.

Akizungumza na wanahabari Sheikh Hemed Jalala, alisema Waislam wa madhehebu ya Shia nchini wamepokea kwa masikitiko makubwa kitendo cha kinyama cha watu kuuawa kwa kuchinjwa hadharani kwa kosa la kutetea dini na haki zao.
“Sheikh Nimr ameuawa kinyama kwa sababu ya kutetea haki za Waislam ikiwemo ya kusali mara tano kwa siku.

Adhabu ya kifo kwa mwanadamu si mafunzo ya Uislamu bali ni uonevu. Naiomba dunia kuingilia kati vitendo vya kinyama vinavyofanywa na serikali ya Saudi Arabia kwa kunyimwa uhuru wa haki za kuishi pamoja na kutoa maoni,” alisema Sheikh Jalala.
Mwanazuoni Ayatollah Sheikh Bagir Nimr aliuwawa Januari, 2 mwaka huu baada ya kutolewa hukumu na serikali ya nchi yake.
(Na Gabriel Ng’osha)
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment