Siku moja baada ya ushindi wa tuzo ya tano ya Ballon d’Or wa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayaeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi, ambaye alikuwa anashindana na Neymar na Cristiano Ronaldo katika tuzo hiyo. January 12 nimekutana hii kutoka sokkaa.com. Mtandao huo umeweka vitu vitano ambavyo vingetokea kama Messi na Ronaldo wangekuwa wanacheza timu moja.
5- Hili ni moja kati ya vitu vinavyotajwa kuwa kama Ronaldo na Messi wangecheza timu moja, basi wachezaji wachanga na chipukizi wangeshindwa kuchagua nani awe Role model wao, Ronaldo na Messi wote wana majina makubwa lakini hii ingeweza kuleta shida kwa wachezaji chipukizi.
4- CR7 na LM10 wangecheza timu moja basi mabeki wa timu pinzani wangekuwa wanaoneshwa kadi nyingi katika mchezo mmoja, kwani kuwakaba wachezaji hao ni kazi ngumu sana. Kwa sasa wanacheza timu tofauti na wanasumbua ngome za ulinzi wa timu pinzani.
3- Timu pinzani ingekuwa ni ngumu kuandaa au kujua ni mbinu ipi sahihi kuwa kaba wachezaji hao. Ronaldo ambaye anacheza Real Madrid na Messi wa FC Barcelona, kama wangekuwa timu moja basi makocha wa timu pinzani wangekuwa na wakati mbadala kutunga mbinu za ulinzi wa wachezaji hao.
2- Uwepo wao kwa pamoja ndani ya kikosi kimoja kingeweza kuleta moral kwa wachezaji na makocha wa timu zao, uwepo wa safu imara ya ushambuliaji wa Lionel Messi na Ronaldo, inaweza kusaidia wachezaji kupata hali ya kujituma na kucheza vizuri na mastaa hao ambao wote wamewahi kushinda tuzo ya Ballon d’Or.
1- Kama Ronaldo na Messi wangekuwa ndani ya kikosi kimoja, basi klabu ingekuwa inachangamoto kubwa ya ulipaji wa mishahara ya wachezaji hao, kwa sasa Messi analipwa mshahara wa euro milioni 20 na Ronaldo analipwa mshahara wa euro milioni 17 kwa mwaka, sasa pata picha hali ingekuwaje kama wangekuwa klabu moja.
0 comments:
Post a Comment