Hii Ndio Heshima Aliyopewa Mbwana SAMATTA na Serikali ya Zanzibar

Bado furaha ya watanzania na serikali kwa ujumla juu ya ushindi wa kihistoria wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe inazidi kushika kasi, tumeona mapokezi ya Samatta aliyoyapata Dar Es Salaam, baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa Ligi za ndani.

January 13 siku ya fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, michuano ambayo inaandaliwa na serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na ZFA, Mbwana Samatta atapewa nafasi ya kuonesha tuzo yake mbele ya wazanzibar, ambao bado wao hawakupata fursa ya kuiona tuzo hiyo toka ashinde.
Samatta pia atapata nafasi ya kuutazama mchezo wa fainali kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya URA ya Uganda katika dimba la Amaan, ambapo mgeni rasmi wa michuano hiyo anatarajiwa kuwa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. Hii itakuwa ni heshima na fursa kubwa kwa Samatta ambaye ataonesha tuzo yake na kupongezwa na wazanzibar wote ikiwemo Rais Shein.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment