Hii ni Kauli ya YAYA TOURE, Baada ya CAF Kumpa Tuzo Pierre-Emerick Aubameyang na Sio Yeye

Mshambuliaji wa kimataifa Gabon ambaye anaichezea klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani Pierre-Emerick Aubameyang ameingia kwenye headlines mara mbili tofauti. Headlines kubwa ya staa huyo ni juu ya ushindi wake wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2015, lakini ya pili ni kuhusu Yaya Toure anavyoamini kuwa Pierre hakustahili tuzo hiyo.

Toure ambaye ni mshindi mara nne mfululizo wa tuzo ya mchezaji bora Afrika, alikuwa na matumaini ya kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya tano ila anashangazwa na shirikisho la soka barani Afrika kudharau mafanikio yake ya kutwaa taji la mataifa ya Afrika na kumpa tuzo Aubameyang, kwani anaamini Kombe hilo halithaminiki.

Pierre -Emerick Aubameyang akikabidhiwa tuzo na rais wa CAF
“Nimesikitishwa sana sana na jambo hili ni aibu kuona Afrika tunavyoichukulia, hatutoi kipaumbele kwa mashindano yetu ya ndani. Nafikiri tumeitia aibu Afrika. Tumeifanya Afrika isionekane muhimu mbele ya macho yetu, tunathamini mafanikio ya nje ya Afrika kuliko ndani ya bara letu”>>> Yaya Toure

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 ameongea hayo baada ya kufanya mahojiano na kituo cha radio cha RFI, nakueleza kushangazwa na ushindi wa Aubameyang katika tuzo hiyo na yeye kupotezewa, licha ya kuwa ametwaa taji la mataifa ya Afrika kama nahodha wa Ivory Coast.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment