Gazeti maarufu la michezo Hispania la Marca, January 12 limepamba headlines zake za gazeti kwa kumuandika kocha anayetajwa kuwa ghali kwa sasa duniani Pep Guardiola na mshindi wa tuzo tano za Ballon d’Or Lionel Messi. Gazeti hilo limewaandika Messi na Pep Guardiola kuwa Adidas inataka kuwaona wakijiunga na klabu ya Man United msimu ujao.
Adidas ambayo ni kampuni ya kijerumani inayojihusisha na utengenezaji vifaa vya michezo duniani, ndio kampuni inayodhamini klabu ya Man United kwa sasa, Pep Guardiola pamoja na Lionel Messi, hivyo inatajwa kuwaweka pamoja ni kuitangaza biashara yao kwa pamoja, tofauti na sasa Messi akiwa FC Barcelona anavaa viatu vya Adidas lakini jezi analazimika kuvaa ya Nike.
Marca limekuwa ni gazeti mahiri la kufichua stori nyingi za ndani za michezo kutoka Uingereza, mpango wa Adidas unaonekana kuwa mgumu, hususani ukizingatia Pep Guardiola anahusishwa kwa karibu na kujiunga na Man City msimu ujao, lakini Lionel Messi nae hapewi nafasi kubwa kuwa anaweza akaondoka FC Barcelona kwa siku za karibuni.
0 comments:
Post a Comment