Staa wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid.
KWA mara ya kwanza staa wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid amefunguka
kuwa yupo mbioni kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Tania
Omotayo.
Wizkid mwenye mtoto mmoja aitwaye Boluwatife amekuwa na uhusiano na
Tania kwa muda mrefu na uhusiano wao umekuwa wa kuachana na kurudiana
lakini amesema hilo halimpi shida kwani Tania yupo moyoni mwake na
itaendelea kuwa hivyo.
Alisema
kuwa hajali maneno yasemwayo kwa baadhi ya wati, mara zote atabakia
kuwa na Tania moyoni mwake na ataendelea kufanya kila liwezekanalo kumpa
mapenzi matamtamu na wasubiri ndoa hivi karibuni. “T (Tania) ni wa moja
kwa moja kwangu.”
Kila la heri, Wizkid katika ndoa yako na Tania.
0 comments:
Post a Comment