Je, Unajua Kinachoendelea Kwa P-SQUARE? Soma Hapa...

PSquare
Paul na Peter, P-Square.
KUNDI la muziki linaloundwa na pacha wawili, Paul na Peter, P-Square huenda linaenda kusambaratika kama inavyoendelea kuanikwa na mashabiki wao.
Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu mmoja wa wanaounda kundi hilo, Peter kufanya kazi kivyake, kumiliki kampuni yake na kutengeneza kipindi chake kiitwacho Dance With Peters maswali mengi yamekuwa yakiibuka na kuuliza kulikoni kwa Paul.

Hivi karibuni, Paul naye ameibuka kivyake na kufanya kazi kivyake ambapo kwa sasa anamiliki kampuni yake ya kurekodia muziki iitwayo Rudeboy Records na kizuri zaidi tayari ameshamsainisha msanii mmoja aitwaye, Muno Sings na wamekuwa karibu kama alivyo Daimond kwa msanii wake Harmonize. 

Katika kuufungua mwaka, Paul aliwaambia mashabiki wake; 
“2016, Muno Sings. Mashabiki wangu kaeni mkao wa kusikia sauti ambayo haijawahi kutokea. Nakuja. Rudeboy Records inaendelea.”
Kisha Paul akasisitiza kwamba hajafanya makosa kabisa katika kuandika jina la Lebo ya Rubeboy na baada ya hapo akashea na mashabiki wake lebo yake hiyo mpya.

Tujikumbushe: Mapema mwaka jana kulitokea mikwaruzo kati ya Peter na Paul huku chanzo kikidaiwa Peter kuingilia ndoa ya Paul.
Bifu lao kubwa jingine ambalo lilikuwa la kimyakimya lilitokea tena mwaka jana baada ya Peter kujitamba katika mitandao ya kijamii kuwa amekuwa akitunga na kuimba nyimbo karibu zote za P-Square.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment