Lamar Odom Aonekana Mitaani Los Angeles

rs_634x1024-131002130843-634.2lamar-odom.ls.10213_copy 
Staa wa zamani wa mpira wa kikapu, Lamar Odom.
STAA wa zamani wa mpira wa kikapu, Lamar Odom ameonekana kuimarika afya yake na kuweza kuzurula mitaani ambapo jana alinaswa mitaa ya Los Angeles.

Picha zinazoendelea kuzagaa zinamuonesha, Lamar (36) akiwa ndani ya gari siti ya mbele na haijajulikana hasa aliyekuwa akimuendesha licha ya kuonekana mara kwa mara wakiwa maeneo hayo yanayosemekana kuna tiba maalum ya waathirika wa madawa ya kulevya.

Staa huyo wa zamani wa Timu ya LA Lakers kwa sasa inasemekana pia anafanya mazoezi ya kutembea peke yake na hata juzi (Januari 6) aliyekuwa mchumba wake ambaye pia ni mdogo wa mwanamitindo, Kim Kardashian, Khloe Kardashian alizungumzia hali ya mchumba wake huyo kwa sasa kwa kusema;
“Najivuni kuimarika kwa afya ya Lamar kitu ambacho nimekuwa nikikipigania kurudisha uhai wake.”
Oktoba 13, mwaka jana, Lamar alinaswa pande za Navada, Marekani akiwa hoi baada ya kubwia madawa ya kulevya kupindukia hali iliyomladhimu kukimbizwa hospitali lakini hali yake kwa sasa imeonekana kuimarika japokuwa bado anaendelea na dozi.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment