Mwimbaji mkongwe, Judith Wambura aka Lady Jaydee ameongeza nguvu
kwenye safu ya uongozi wake ili kujiweka vizuri zaidi katika muziki
wake.
Akizungumza na Bongo5 leo, mmoja kati ya wanaounda uongozi huo, rapper Wakazi amesema amemwongeza Seven katika timu yake.
“Kwa upande wa uongozi wa Lady Jaydee siko peke yangu, nipo mimi na
Seven naye anahusika kwenye uongozi. Lakini Lady Jaydee amepumzika na
bado anaingia studio. Pia bado ngoma yake aliyofanya na Uhuru pamoja
Mazet, ‘Give Me Love’ inafanya vizuri,” amesema.
“Hivi ninavyoongea tarehe 5 ana show Uingereza.”
0 comments:
Post a Comment