Adhabu ya LORD EYEZ Ilishaisha Lakini Hatujui Kwanini Bado Haonekani Ofisini – WEUSI

Lord Eyez ni mmoja wa wasanii wa kundi na kampuni ya Weusi hadi sasa, lakini ni muda mrefu hajaonekana wala kazi zake kusikika kama wenzake kina Joh Makini, Nikki Wa Pili, Bonta na G-Nako.
Maswali ambayo Weusi wamekuwa wakiulizwa kuhusu Lord Eyez ni kuhusu kama bado yuko nao na kwanini hajasikika kwa muda mrefu.

Mwezi March mwaka huu Weusi walimsimamisha Lord Eyez kikazi kutokana na kukiuka maadili na sheria za kampuni yao, kufuatia taarifa kuwa alikamatwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa laptop huko Arusha. 

Nikki wa Pili ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa Lord Eyez amemaliza adhabu yake lakini hawajui kwanini hataki kujumuika nao kufanya kazi wala hatoi kazi mpya.
“Lord Eyez kwakweli niseme kila kitu kiko kwenye mikono yake kwasababu mambo yake na kampuni alishaya-settle yalishaisha, lakini yeye alienda Arusha nafikiri saizi kama Mwaka alisema anapumzika kidogo…Lakini so far kwa maelezo yoyote saizi nafikiri labda Lord Eyez mwenyewe angetafutwa angeweza kusema vizuri, lakini sisi kwa upande wa kampuni adhabu yake na kila kitu vilishaisha.” alisema Nikki wa Pili 

Nikki ameongeza kuwa upande wa uhusiano wa Lord Eyez na members wengine wa Weusi nje ya muziki kila kitu kiko sawa kwa sasa.
“Hakuna tatizo lolote kati ya yeye na kampuni yaani either kiurafiki, kiundugu vile tunavyoishi kla kitu ni kama zamani.” Alisema Nikki.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment