Lagos, Nigeria
MASTAA wa muziki wa Nigeria,
ambao pia wamekuwa mahasimu kutokana na kazi zao wanazofanya kufanana na
kujitwalia mashabiki kibao, Davido na Wizkid wamethibitisha kumaliza
kabisa tofauti zao baada ya kupanda na kutumbuiza kwenye jukwaa moja
wakati wa shoo iliyofanyika Alhamisi Desemba 3, mwaka huu jijini Lagos,
Nigeria.
Uthibitisho wa kumalizika kwa tofauti
zao ni kutokana na video ya shoo hiyo ya club iliyosambaa mitandaoni
ikumuonesha Davido ndiye aliyekuwa wa kwanza kupanda jukwaani na kuanza
kuimba wimbo wake wa ‘Dami Duro’.
Wakati akielekea kumaliza kuimba wimbo
huo, ghafla Wizkid naye alitokea upande wa mashabiki kabla ya Davido
kumpokea kwa kumvuta mkono kisha wote kupanda jukwaani na kuendelea
kuimba pamoja nyimbo zote zilizofata bila kushuka.
0 comments:
Post a Comment