VANESSA MDEE Kuanza Kuvumbua na Kusimamia Vipaji Vingine

Wasanii wanaofanikiwa nchini wameonekana kutofaidi mafanikio yao wao wenyewe na badala yake wameanza kusaidia vipaji vingine.
Baada ya Diamond kuanzisha label yake ya WCB ambayo tayari imefanikiwa kumweka kwenye ramani Harmonize, Vanessa Mdee naye ataanza kufanya hivyo hivi karibuni.
Tayari ameanzisha kampuni yake, Mdee Music ambayo licha ya kusimamia kazi zake mwenyewe, itaanza pia kuvumbua na kusimamia vipaji vingine. 

Vanessa ameiambia Bongo5 jana kuwa kampuni hiyo itakuwa ikifanya pia shughuli za utoaji ushauri katika masuala ya burudani.
“We will soon be managing and recruiting new talent as well as consultancy in this field,” alijibu Vanessa tuliyemuuliza kupitia session ya maswali iliyoandaliwa kwenye Twitter na Coke Studio Nigeria.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment