New York, Marekani
TAARIFA zilizoenea kwa kasi kuwa mcheza tenisi namba
moja duniani, Serena Williams ana ujauzito wa rapa Drake Graham,
zimekanushwa vikali.
Hivi
karibuni, iliripotiwa kuwa Serena tayari ameshanasa ujauzito wa Drake
na kwamba dalili zote za mimba kwa mlimbwende huyo zimeanza kubainika
kabla ya hivi karibuni watu wa karibu na staa huyo kueleza ukweli juu ya
suala hilo.
“Serena hajafurahishwa na taarifa hizi zinazopotosha, huwa anatuambia
jinsi gani anajisikia. Ukweli ni kwamba hana ujauzito na ni muda mfupi
tangu akutane na Drake kwenye ‘event’ moja kubwa New York, kwa kifupi
hakuna ukweli wowote,” alisema mmoja wa marafiki wa karibu na Serena.
0 comments:
Post a Comment