LICHA ya muziki wa Bongo Fleva kupiga hatua kubwa hapa nchini,
kumekuwa na athari kubwa kwa maprodyuza wa hapa Bongo kutokana na
wasanii hao kukimbia kufanya ‘chupa’ zao hapa nchini, badala yake
wanakimbilia nje, hasa Afrika Kusini na Nigeria.
Wasanii wengi wanaopenda kufanya video zao nje ya nchi, wamekuwa
wakitoa sababu mbalimbali ikiwemo ubora wa vifaa, kutafuta chaneli za
kuonekana kimataifa zaidi pamoja na mazingira mazuri kwa ajili ya video
hizo.
Tayari kuna wasanii ambao wameonekana dhahiri shahiri kunogewa
kufanya video kwenye nchi hizo na pengine wanaweza kupotea kabisa
mikononi mwa ‘Madairekta’ wa Bongo na kuishia kuwasikia tu.
Makala haya yanakuchambulia baadhi ya wasanii ambao kwa hakika
inaonyesha ipo kazi kubwa kuwashawishi warudi kutengeneza video hapa
nchini kutokana na kauli zao na hata maono yao:
Joh Makini
Anatamba na Wimbo wa Don’t Bother aliomshirikisha staa wa Sauz, AKA
ambapo kideo cha wimbo huo kimefanyika katika ardhi hiyo ya Mzee Madiba
chini ya Justin Campos na kampuni yake ya Gorilla Films.
Kabla ya kufanya Don’t Bother, Joh pia alifanya video ya Nusunusu
nchini humo na kuonekana kutusua vilivyo, hivyo inaonyesha itakuwa kazi
kubwa kumrejesha tena Bongo na kufanya kazi hapa nchini kama ilivyokuwa
kwa kazi zake za mwisho ku-shoot nyumbani za XO na Bye Bye.
Diamond
Huyu ni miongoni mwa waliokataa kufanya video zake nchini, amelowea
Afrika Kusini kwa Godfather ambapo huko amefanyia kideo cha Nana
aliomshirikisha Flavour kutoka Nigeria. Kabla ya hapo Mdogomdogo,
Ntampata Wapi nazo zilifanyika hukohuko na Number One Remix akaifanyia
Nigeria.
Mafanikio anayoendelea kupata kupitia video hizo, si kazi rahisi
kumvuta kufanya video nchini kama awali alipofanya za Mbagala, Kamwambie
na nyinginezo.
Vanessa Mdee.
Vanessa Mdee
Alianza harakati za kuimba kama masihara alipotoa Wimbo wa Closer chini ya Studio za B Hitz lakini leo anatusua vilivyo katika anga la muziki kimataifa huku Never Ever aliyoachia hivi karibuni ikizidi kumbeba.
Vanessa au Vee Money naye ni mmoja wa wasanii waliopo katika listi ya waliokimbia kutoa video hapa nchini, naye amepata mafanikio zaidi baada ya kuanza kazi na waongozaji wa Afrika Kusini.

Navy Kenzo
Ni kundi linaloundwa na wasanii wawili, Nahreel na Aika ambao wamekuwa wakitamba na nyimbo mbalimbali lakini kwa sasa wimbo na ubora wa video yao ya Game walioifanyia Sauz ndiyo unawang’arisha hapa nchini na mipaka ya nje ya nchi.
Tayari wameshaonja utamu wa kufanya video nje ya nchi ambapo Game sasa inachezwa katika vituo vikubwa vya hapa Afrika, ikiwemo MTV Base, Sound City, E na stesheni nyingine nyingi maarufu, kwa walipofika ni ngumu kuwarudisha nyumbani kufanya video zao.

Ali Kiba
Tayari ameshafanya video mbili za nyimbo zake nchini Afrika Kusini;
Mwana iliyotengenezwa na Godfather na Chekecha Cheketua chini ya
dairekta mwenye heshima Afrika, Meji Alabi.
Kutokana na ushindani mkubwa uliopo baina yake na Diamond, inatakiwa
kazi ya ziada kumwambia Kiba arejee na kufanya video zake hapa nchini
kama ilivyokuwa miaka iliyopita kwenye video za Usiniseme, Cinderela na
nyinginezo kwa kuwa tayari ameshaanza kutengeneza njia kubwa zaidi ya
kutusua kimataifa.
Wengine
Wengine
Wengine wanaoonekana kukomaa nchi za nje kutanua ‘carrier’ zao kwa
kufanya video kali ingawa si kwa wingi ni pamoja na Linah, A.Y, Ommy
Dimpoz, Shettah, Yamoto Band, Madee, Temba na Chegge na wengine wengi
wanaozidi kufululiza safari za Sauz na Nigeria kuhangaikia ‘michongo’.
0 comments:
Post a Comment