Mdada Shtuka! AIBU Kwa Mumeo ni Sumu, Ziache Tafadhali...Chumbani ni KAZI TU! Jifunze Zaidi Hapa...

KARIBU wapendwa wasomaji wa safu hii. Bila shaka mlipata somo zuri katika mada ya wiki iliyopita, kwani nilipata ujumbe wa wasomaji wengi, wakielezea kuguswa kwao na kilichoandikwa huku baadhi yao, wakiomba ‘darasa’ la jinsi gani ya kuweza kumhifadhi mume ili kuifanya ndoa iwe na amani.

Kwa kuheshimu maoni yenu, maana kimsingi nyinyi ndiyo hasa wadau wa safu hii, nimeonelea siyo jambo baya nikiwadokolea mambo machache, lakini muhimu ninayoyajua, ambayo yanasaidia sana kumhifadhi mume na hivyo kuifanya ndoa yako kuwa imara kadiri siku zinavyokuja na kuondoka.

Mojawapo ya jambo linalokosewa na wengi wetu ni aibu kwa waume zetu, hasa tunapokuwa nao faragha. Hivi mtu unamuoneaje aibu mumeo chumbani jamani, kwani ni nani wako yule, mjomba au mzazi?

Aibu hii ndiyo huwafanya wengine wawaache bila kuwasumbua waume zao, kwa sababu tu wamekuja wamelewa au wamechelewa kuwasili nyumbani. Nakwambia hivi, usithubutu kumuacha akalala wakati wewe unamhitaji, utajikuta unaumiza nafsi yako bure, kwa nini uumie wakati wa kukupoza yupo?


Fanya hivi 
Mpokee vizuri na umchojoe nguo zake zote, kisha mpeleke bafuni uhakikishe ameoga, ukimaliza muulize kama atapata chochote cha kula, maana kuna wengine wakishapata kinywaji ni nadra kula, lakini pia mpeleke taratibu mpaka akubaliane na hali yako.

Kumbuka
Mume kulala na nguo hilo ni kosa lako mwanamke, unatakiwa kumpa mapokezi mumeo pale tu anapotoka kazini au kwenye mihangaiko yake popote bila kujali amerudi na nini au alienda kufanya nini.

Ukishamaliza sasa anza kumhangaisha kwa kumgusa sehemu unazohisi zinaweza kumkumbusha nini unahitaji, katika hali ya kawaida, lazima ataonesha ushirikiano. Na ikitokea ‘ameingia line’, acha aibu, onesha uwezo wako kwa manjonjo yote unayojua.

Wanawake wengi wana aibu kuwaonesha waume zao mahaba, hasa kama anamuhitaji eti atamuona ana uchu, hivi usipokuwa muwazi kwa mumeo, unataka huo uwazi ukamuoneshe nani?

Shosti, usijali, jaribu kuwa mapepe kwa mumeo na awe mumeo tu uone, kwa sababu wapo baadhi ya waume zetu wanatoka nje kwa sababu wanawake wa nje ni mapepe, yaani wehu kabisa wawapo chumbani.

Utasikia mwanamke anasema mimi siwezi kumchojolea mume labda kuwe na giza, nikwambie, wanaoiweza ndoa wote wakiwa ndani na wapenzi wao wanajiachia vilivyo.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment