Mtangazaji mahiri wa kipindi cha XXL cha Clouds FM, Hamis Mandi aka B12 amesema watu wengi humfirikia tofauti na alivyo.
B-Dozen amesema watu wengi huhisi ni mtu mwenye kujisikia na asiyependa kujichanganya na watu.
“Watu hunifikiria tofuti na nilivyo,” Dozen ameliambia gazeti la
Mwananchi. “Mimi ni mtu mwenye aibu sana. Mara nyingi kama mtu simjui
vizuri inanipa wakati mgumu kutoa ushirikiano kutokana na kuwa huwa
najishtukia,” aliongeza.
“Sio kama najitenga ni udhaifu wangu unasababisha watu kunidhania
ndivyo sivyo. Lakini kwa wanaonijua vizuri wanajua mimi ni mshikaji
sana.”
0 comments:
Post a Comment