Musa Mateja
NI gumzo! Ubuyu motomoto ambao
unasambaa kwa kasi ya ajabu kama moto wa kifuu mjini unadai kuwa, staa
nambari moja Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwigizaji
Kajala Masanja wamedaiwa kuwa ni wapenzi na sasa ni mahaba niue, Risasi
Jumamosi limesheheni full stori.
TUJIUNGE NA CHANZO
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, uhusiano wa
Diamond na Kajala unadaiwa kuibuka ghafla miezi kadhaa iliyopita
lakini wamekuwa wakifanya siri nzito kabla ya hivi karibuni kukolea
zaidi baada ya mpenzi wa Diamond, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’
kurudi nchini mwake, Afrika Kusini ‘Sauz’.
“Walianza zile za kimjinimjini, wakawa
wanafanya yao kimyakimya tangu Zari akiwepo lakini mahaba niue yamekuja
kushamiri zaidi baada ya Zari kutimkia zake Sauz,” kilisema chanzo
chetu.
MASTAA WAZUNGUMZIA
Mara baada ya chanzo hicho kumwaga ubuyu
huo, Risasi Jumamosi lilipenyezewa data kutoka kwa mastaa tofauti ambao
wanafahamu uhusiano huo mpya ambao pia ulianza kusambaa taratibu katika
mitandao ya kijamii.
“Hivi kwani nyinyi hamjaipata habari
hii? Diamond amemnasa Kajala na mambo yao ni bambam. Sema kiukweli
Diamond ni msiri maana unajua ana mambo mengi hivyo hapendi kabisa hii
ishu ijulikane,” alisema staa mmoja mkubwa Bongo huku akiomba hifadhi ya
jina.
Kama hiyo haitoshi, staa mwingine
aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, dada wa Diamond, Esma anaujua mchezo
mzima na anatajwa kuusambaza ubuyu huo kama malipo kwa Wema (Sepetu)
anayemtuhumu kumuibia bwana wake, Petit Man.
“Esma ameamua kumwaga ugali maana Wema
na timu yake wamekuwa wakijitapa sana mjini kwamba wamemnyakua mume wa
Esma, Petit Man. Na yeye anawaonesha kwamba kama ni kuchukuliwa mbona
hata Kajala amechukuliwa na Diamond ambaye alikuwa mtu wa Wema lakini
wamekaa kimya,” alisema msanii huyo.
Jitihada za kumpata Esma ili aweze
kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba baada ya simu yake ya mkononi
kuita muda mrefu bila kupokelewa.
MITANDAO YAZIDI KUKUZA JAMBO
MITANDAO YAZIDI KUKUZA JAMBO
Mpaka tunakwenda mitamboni, juzi,
mitandao mbalimbali hususan Instagram, wadau walisambaza habari ya
Kajala na Diamond huku wakijaribu kumwambia Zari amtambue Kajala kama
mke mwenzie kwani ameshalala Madale, nyumbani kwa Diamond.
“Zari mke mwenzio ni huyu hapa, anakusaidia. Juzi amelala Madale na Diamond,” iliandikwa na mdau mmoja wa Instangram.
ZARI ACHANGANYIKIWA
ZARI ACHANGANYIKIWA
Chanzo kilichomwaga ubuyu huo kimeeleza
kuwa, taarifa za Kajala na Diamond zilipomfikia Zari, alichanganyikiwa
na kuanza kumcharukia Diamond au baba Tiffah ambaye ilibidi atumie nguvu
ya ziada kumtuliza kwani bado wawili hao wanaendeleza uhusiano wao huku
wakijua Zari hayupo Bongo.
“Zari alicharuka kwelikweli. Ilibidi
Diamond atumie nguvu ya ziada kumtuliza na bahati nzuri mtoto wa kike
ameelewa,” kilisema chanzo chetu.
DIAMOND SASA
DIAMOND SASA
Alipotafutwa Diamond na kusomewa mashitaka yake, mambo yalikuwa hivi:
Risasi Jumamosi: Kuna
taarifa kwamba unatembea na Kajala na sasa mahaba ni motomoto, vipi kuna
ukweli? Tena vyanzo vingine vinadai kuna hadi picha za wewe na Kajala
mkiwa nyumbani kwako, unazungumziaje hilo?
Diamond: Aaah! Siyo kweli mwanangu…picha kweli mnazo? Picha gani…yaani kiaje?
Risasi Jumamosi: Inasemekana zipo ambazo mpo nyumbani kwako, Madale.
Diamond: Aahaha! Aaah uongo mtupu siyo kweli. Kama kuna picha kweli nitumieni basi.
KAJALA SASA
KAJALA SASA
Alipopigiwa simu zaidi ya mara tano, Kajala hakupokea. Risasi Jumamosi lilimtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) uliosomeka hivi:
“Habari, kuna ishu yako hapa Global
Publishers, inahusu madai ya wewe kutoka kimapenzi na Diamond jambo
ambalo linadaiwa kuleta mtafaruku mkubwa kati yako na Zari. Pia hata
kwenye mitandao ya kijamii bila shaka umesikia, naomba ufafanuzi wako
tafadhari.”
Licha ya ujumbe huo kuonesha kumfikia, hadi tunakwenda mitamboni, Kajala hakujibu chochote.
KAMA NI HIVYO
KAMA NI HIVYO
Madai ya kuwepo kwa uhusiano huo
yanaweza kumweka Kajala katika mtazamo mwingine kijamii, kwani miaka
miwili nyuma alidaiwa kutoka kimapenzi na mwanaume anayeitwa CK ambaye
hakuna shaka alikuwa mpenzi wa Wema kabla ya kumwagana.
Hali hiyo ilizua mjadala, Kajala
alibebeshwa madai mazito kwamba alikuwa na uhusiano na CK hata akiwa na
Wema, ikitafsiriwa kwamba alikuwa akimlia vyake mwenzake hali iliyozua
mgogoro wa wawili hao.
Diamond naye, amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema, wakamwagana. Kitendo cha kudaiwa kutoka na Kajala, kinazidi kumweka mdada huyo katika mlolongo wa kudhaniwa anamwandama Wema kwa vile kila alikopita, yeye naye anapita!
Diamond naye, amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema, wakamwagana. Kitendo cha kudaiwa kutoka na Kajala, kinazidi kumweka mdada huyo katika mlolongo wa kudhaniwa anamwandama Wema kwa vile kila alikopita, yeye naye anapita!
0 comments:
Post a Comment