Mkongwe wa Bongo Movies, Jimmy Mafufu.
Imelda Mtema
HATARI! Mkongwe wa Bongo Movies, Jimmy
Mafufu ameonesha hisia kali baada ya kutoa kiapo kuwa hatahudhuria msiba
wa msanii yeyote, hata afe Vincent Kigosi ‘Ray’ kufuatia wasanii
kutompa ushirikiano wakati wa kifo na mazishi ya marehemu baba yake
mzazi, Mchungaji Mafufu.
Akizungumza na gazeti hili kwa uchungu,
Mafufu alisema hivi karibuni alifiwa na baba yake mzazi lakini aliumizwa
sana baada ya kupigiwa simu ya pole na wasanii wawili tu, wakati yeye
muda wote alijitoa kwenye misiba ya wenzake.
“Jamani sikuwa najua wanadamu ndivyo
tulivyo, mimi ikitokea kuna msiba kapata msanii mwenzangu, ni rahisi
kuwakusanya wasanii wenzangu Leaders na hata kuchangishana lakini kwangu
kumekuwa kama hakuna kitu kilichotokea kabisa, nimepigiwa simu na JB na
Wolper peke yao,” alisema Mafufu.
Kutokana na hali hiyo, Mafufu alisema
hatakanyaga kwenye msiba wa msanii yeyote, awe Steve Nyerere, Aunt
Ezekiel, Johari au wengine kwa kuwa amejifunza kwa alivyofanyiwa.
“Yaani hili ni tamko rasmi, sitakanyaga
kabisa kwenye msiba wa msanii yeyote, afe Ray, Aunt, Johari na yeyote
yule sitokanyaga kabisa” alimalizia Mafufu.
0 comments:
Post a Comment