Diamond Platnumz ametokea kuwa balozi mzuri wa lugha ya Kiswahili, kwasababu mafanikio aliyonayo sasa ya kufanya vizuri ndani na nje ya Afrika yametokana na nyimbo za Kiswahili alizotoa hadi sasa.
Baada ya kugundua kuwa kinachoweza kusababisha wimbo upendwe kimataifa sio lugha, hit maker huyo wa ‘Nana’ hana mpango kabisa wa kurekodi nyimbo za Kiingereza, licha ya kuwa ameshawahi kutoa wimbo wa Kiingereza, collabo yake na Iyanya ‘Bum Bum’ ambayo hata hivyo haikufanya vizuri kama nyimbo zake za Kiswahili.
“Hatuwazi kabisa kufanya nyimbo ya kizungu kwasababu Kiswahili ndicho kimetufanya tukavuka boda,” alisema Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond kupitia 255 ya XXL. “sio ushamba kutokuimba kizungu…Cabo Snoopy haimbi kizungu yule anaimba kikwao, wapo wakubwa kibao ambao wanaishi Ufaransa wanaimba Kifaransa wanaoishi Portugal wanaimba ki Portuguese, yaani hivyo, unatokea Tanzania imba Kiswahili, hata tukifika Nigeria wakimwona Diamond anafanya Interview ya kizungu wanamshangaa, wapo wanaokwenda pale hawajui hata kuongea kizungu…basi sometimes wanamuomba awafundishe maneno machache ya Kiswahili, ni dalili nzuri ya kutangaza lugha yetu.” alisema Tale.
Tale aliendelea kusema;
Msanii mwingine wa Afrika ambaye ameshaweka msimamo kuwa hatatumia kiingereza kwenye nyimbo zake ni rapper Sarkodie wa Ghana.
Sarkodie hutumia lugha ya kwao kwa kuchanganya na Kiingereza kidogo sana, lakini ni msanii ambaye ameshashinda tuzo mbalimbali kubwa kama ya BET Awards 2012 ‘Best International Act’, na ameshapata nominations za MTV MAMA, Channel O Music Awards, MOBO, AFRIMMA na zingine, kutokana na nyimbo hizo hizo.
0 comments:
Post a Comment