Abdul KIBA: Kubaniana Kunakatisha Tamaa

IMG-20150522-WA0038Msanii wa Bongo Fleva Abdul Kiba.
Chande Abdallah
Msanii wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Ayaya aliomshirikisha mwanadada Ruby, Abdul Kiba, ameonesha kusikitishwa na hali iliyopo nchini ya wasanii waliofika mbali kimuziki kuwazibia wasanii wengine wasifikie walipo wao na kufunguka kuwa hali hiyo inakatisha tamaa.

Akikazia kauli ya kaka yake, Ali Kiba ambaye alifunguka hivi karibuni kuhusu ‘ufisadi’ huo unaofanywa na wasanii wenzao wanaochukua tuzo kila kukicha, Abdul Kiba alisema kuwa wasanii hao wanapaswa kuwa wazalendo na wanapaswa kuwaiga wasanii wenzao kutoka Nigeria ambao wanapeana sapoti kubwa bila kujali ustaa wao.
“Lazima tusaidiane tukue, wote tunahangaika siyo vizuri tuuane nguvu, wenzetu Nigeria wanapeana njia, hapa unakuta watu wanakuzibia hadi basi,” alisema Abdul Kiba.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment