Bila kuwachosha zaidi niende kwenye mada moja kwa moja, mada hii ina lengo la kuwahusia akina mama wote wanaojishughulisha na simu ya mume/mpenzi, huu unaitwa ulimbukeni.
Unadhani ndiyo unampenda sana
Hivi kupekua simu ya mume au mpenzi au kumnyima raha ya kuongea na watu unadhani ndiyo kumpenda sana? Au kumkarahisha, huo nasema ni ulimbukeni wanawake wenzangu leo nataka niwape somo na liwaingie hasa.
Nimeamua kuandika mada hii kwa sababu ya mwanaume mmoja ambaye amenitumia ujumbe mfupi wa maneno akiniuliza hivi mwanamke kukufuatilia kwa kuchunguza simu ndiyo anaonesha kumpenda sana? Hakuishia hapo aliendelea kusema kuwa yeye anavyoona muda si mrefu ndoa yake itavunjika kwa sababu ya simu.
Hivi uachwe kwa sababu ya simu?
Unaachwaje kwa sababu ya simu, kumbuka kuwa mwanaume ni binadamu na binadamu huwezi kumchunga kwa njia yoyote ile labda apende mwenyewe kwani hata wewe si rahisi kukuchunga sasa simu isije kukufanya ukaonekana wa ajabu kwa kuachwa.
Mwanamke jiamini
Mwanamke umeshapewa himaya kwa nini usijiamini, unayumba kwa ajili ya simu, hivi ukijikuta unadanganywa na ulishaaminishwa kwa simu utafanya nini? Kwa sababu maisha ya mwanaume hayapo kwenye simu tu, kama unahisi unampenda sana kwa nini usiende naye kila kona ili kumlinda vizuri.
Uaminifu ndiyo kinga kuu
Jenga tabia ya kumuamini mume na ndiyo itakupa ujasiri wa kuishi kwenye ndoa yako milele, nikuambie tu siri ya ndoa kudumu ni pamoja na wanandoa kuaminiana.
Ukimuamini sana mume kwa kutomfuatafuata hata akikufanyia jambo baya ni rahisi kulijutia na kukuomba msamaha lakini iwapo utakuwa ni mtu wa kumfuatilia nyendo zake siku akikukosea pia ni rahisi kukwambia kuwa alifanya hivyo ili kukukomoa sasa utakuwa umejenga au umebomoa? Jifunze mwanamke.
Simu zimevunja ndoa za watu na mtu akikaa kando ndiyo anajishangaa kwani simu ni kitu kidogo ambacho ukikidharau utadumu kwenye ndoa yako kwa muda mrefu na kumbuka simu siyo mlinzi wako, ulinzi ni matendo yako kwa mumeo tu.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment