Hii ngoma audio yake ilifanyika hapahapa Tanzania mwishoni mwa mwezi April 2015 wakati ambao rapper AKA alitua baada ya kupata mwaliko wa party ya Zari All White iliyoandaliwa na mastaa wawili wapenzi, Diamond Platnumz na Zarina Hassan a.k.a Zari the Boss Lady.
Wazo la collabo ya rappers wawili likaibuka, wakakutana member wa kundi la Weusi, Joh Makini na rapper AKA kutoka South Africa… Producer Nahreel akaikamilisha kazi yote ya audio, mipango ya video ikafatia.
Kitu kimeachiwa tayari, kazi yote imefanyika South Africa chini ya Director ambaye tayari kuna list kubwa ya video nzuri zilizopitia kwenye mikono yake, Justin Campos… Yes yes, time nyingine ndio hii mtu wako wa nguvu nakusogezea hii kwenye dakika zake tatu hapa chini… Joh Makini Feat. AKA– ‘Don’t Bother‘.
0 comments:
Post a Comment