Najua ukitaja list ya mashujaa wa kike
ambao wamekuwa kwenye headlines za kuibeba Bongo Fleva kwenye mipaka nje
ya Afrika na Dunia, jina la Vanessa Mdee a.k.a ‘Vee Money‘ lazima litakumbukwa pia.
Vee Money amefika
kwenye nafasi ya kuwa kwenye list ya nominees kwenye tuzo mbalimbali
kubwa Afrika na duniani lakini hayo matunda yote ni ndani ya kipindi cha
miaka miwili tu aliyoamua kwamba anaweka nguvu yake yote kwenye muziki.
Countdown ya Tuzo za AFRIMA 2015
inaendelea kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, kama hujajua basi hii ikufikie
kwamba zimebaki siku tatu tu kuifikia November 15 2015 ambapo
tutamshuhudia Vanessa Mdee akiperform kwenye stage moja na wakali wengine wa Afrika ikiwemo kundi la Ladysmith Black Mambazo kutoka South Africa.
Fainali ya tuzo hizo itakuwa katika Jiji la Lagos Nigeria, na hitsong ya ‘Hawajui’ ya Vee Money imekuwa nominated kwenye category ya Best African Pop Song, vilevile jina lake lipo pia kwenye ngoma ya collabo ya ‘Strong Girl‘ ambayo inawania tuzo pia kwenye category ya Best Collaboration ambayo ndani yake wamo akina Yemi Alade, Waje na Victoria Kimani.
Kila la heri kwa mtu wetu Vee Money kwenye safari ya kuelekea Lagos Nigeria ambako zinatolewa Tuzo za AFRIMA 2015.
Hit mpya ni hii, ‘Never Ever‘- Vanessa Mdee kwenye ubora wake.
0 comments:
Post a Comment