Q-Chief amesema tayari amesharekodi wimbo wa pamoja na swahiba wake
TID na sasa yupo kwenye mazungumzo na Diamond Platnumz kuhakikisha
anaibariki pia ngoma hiyo.
Q amesema baada ya kuona wamemaliza tofauti zao, alimshauri TID
kufanya wimbo wa pamoja kama wasanii wakongwe wa muziki wa Bongo Flava.
“Nimerekodi na TID ambaye tulikuwa tuna mgogoro ndani ya miaka 6 au 7 na
kila mtu anajua,” Q-Chief ameiambia Bongo5.
“Lakini tumemaliza tofauti zetu, sisi kama watu wazima tunajitambua
na nikamwambia hebu tujaribu kufanya ngoma fulani kama aina ya mdumange,
ili tujaribu kurudi nyumbani kwa watu wetu. Na ukiangalia wasanii wa
kwanza waliofanya vizuri ni Q Chillah na TID.”
“Kwahiyo tumefanya project kwa Abby Daddy, na Abby Daddy naye yupo
kwenye mazungumzo na Diamond ilikuwa aingie kwenye hii ngoma. Tayari TID
amemtumia ngoma kwa sababu ametoka kuchukua zile tuzo inabidi
tumpongeze halafu tumpe kama wiki moja na nusu then tujue kama ataingia
au vipi. Kwa sababu tunajua anaweza kuwa busy sana lakini ile ngoma
tayari ni hit. Kwahiyo mwezi wa kumi na moja watu watapata vitu vizuri.”
0 comments:
Post a Comment