Roma Mkatoliki ameamua kuchukua jukumu la kwenda Baraza La Sanaa
Tanzania, BASATA kuwasikilizisha wimbo wake mpya anaotarajia kuuachia
Jumapili siku ya uchaguzi Oct.25 ili waupe baraka kuepuka kufungiwa.
Uamuzi huo umekuja kutokana na misukosuko aliyokutana nayo baada ya
kutoa wimbo wake wa ‘Viva Roma Viva’ hivi karibuni, ambao BASATA
waliufungia kutokana na madai kuwa hakuna ushahidi wa vitu vilivyoimbwa
kwenye wimbo huo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Roma alipost ujumbe huu siku ya Jumamosi Oct.24;
“Kesho Ndiyo Ile Tarehe Niliyowaahidi
Kuwa Nitaachia #KIBAO Changu Kipya!!!!! /
Na Sasa Naelekea #BASATA Kuwasikilizisha Kabisa Kwanza!!! Wakitoa#GO_A_HEAD Tu Basi Kesho Alfajiri #KINANUKA /
WAKIZINGUA NA MIMI NAWAZINGUA!!! /”
Kuwa Nitaachia #KIBAO Changu Kipya!!!!! /
Na Sasa Naelekea #BASATA Kuwasikilizisha Kabisa Kwanza!!! Wakitoa#GO_A_HEAD Tu Basi Kesho Alfajiri #KINANUKA /
WAKIZINGUA NA MIMI NAWAZINGUA!!! /”
0 comments:
Post a Comment