Juma Nature amesema hana haraka ya kwenda kimataifa kwa kudai bado ana muda wa kutosha kwenda huko.
Nature anadai kuwa bado anajichukulia kama msanii mchanga mwenye kipaji cha ajabu.
“Hizo ni plan zangu baadaye sio sasa hivi,” Nature ameiambia Bongo5.
“Mimi sifanyagi kitu kwa kuiga, kwa sababu mimi sio underground na
nina jina la kutosha lakini unaweza kunifananisha na underground mwenye
kipaji. Nikiona watu wanashindwa kufanya vizuri nakaza ili niwaonyeshe
Nature ni nani! Kwa sababu mimi kimataifa nilishafika huko wakati wa
nyuma, kwahiyo mimi sio mshamba wa maisha hapa duniani. Vingi nimefanya
kupitia sanaa kwahiyo hivyo wanavyofanya wenzangu naona ni mambo ya
kawaida tu,” amesisitiza.
0 comments:
Post a Comment