Mwigizaji superstar wa Nigeria, Genevieve Nnaji amezungumzia kuhusu maisha yake ya mapenzi na mipango ya ndoa.
Genevieve ni msichana mrembo na aliyefanikiwa kimaisha kupitia filamu pamoja na biashara zake nyingine ikiwemo mitindo, lakini katika umri wa miaka 36 alionao sasa bado hajabahatika kuolewa.
Staa huyo ambaye kwa sasa anapromote filamu yake mpya ‘Road To
Yesterday’ ametoa sababu ambayo hutolewa na mastaa wengi ambao hawajaoa
au kuolewa, kuwa hadi sasa bado hajaolewa kwasababu hajapata mwanaume
anayemfaa.
Akizungumza na Punch, Genevieve amesema kuwa ‘mr right’ atakapojitokeza basi atafunga pingu za maisha.
“I haven’t found the right man yet. When he comes, I’ll get married” – Nnaji
0 comments:
Post a Comment