Mikel Ruffinelli ndiye mwanamke anayejulikana rasmi kuwa na ‘mahips’ makubwa zaidi duniani.
MIKEL RUFFINELLI ndiye mwanamke mwenye ‘mahips’ (nyonga au makalio) makubwa zaidi duniani hivi sasa na ameingia katika Kitabu cha Kumbukumbu za Dunia cha Guinness.
Mama huyo ambaye ni Mmarekani, anasema anajisikia raha mustarehe na umbo lake hilo alilo nalo.
Ruffinelli ambaye ni mama wa watoto wanne, mkazi wa Jimbo la California, Marekani, anasema anaishi maisha ya kawaida na kuendesha kazi zake vizuri ambapo mumewe, Reggie Brooks, pia humsifia kwamba anampenda jinsi alivyoumbika.
Kwa mujibu wa gazeti la ‘WorldWide Werid News’, Ruffinelli alikuwa na umbo la kawaida kabisa wakati wa ujana na hakuwa na tatizo lolote la kuongezeka uzito, lakini, akiwa na umri wa miaka 22, alianza kuona ‘mahips’ yake yanazidi kuongezeka baada ya kuzaa mtoto wake wa kwanza.
Aliongeza kusema kwamba kila alipokuwa anazaa, sehemu yake hiyo ya mwili ilizidi kuongezeka mpaka akawa anashindwa kupita kwenye mlango wa kawaida. Japokuwa kiuno chake kina inchi 40 (sentimita 102), nyonga zake zinafikia inchi 100 (sentimita 254), hali inayomfanya avunje rekodi ya dunia.
Umbo lake humlazimu kupita kiubavu katika milango mbalimbali na huwa hawezi kufunga mlango wa bafu lake wakati akioga kwani sehemu ya mwili wake huwa imejitokeza nje.
HABARI NJEMA! MODEL WA TZ, HAPPINESS MAGESE NDANI YA VIDEO YA MSANII WA KIMATAIFA!
===>>SHUHUDIA HAPA! PATA HABARI HARAKA ZITUFIKIAPO.
===>>SHUHUDIA HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO
TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142
KARIBU TENA!

0 comments:
Post a Comment