MAAJABU YA MTWARA: ETI WAZUNGU WAFANYIWA TAMBIKO! -PICHAZ

Bosi wa kampuni ya mafuta ya Maurel et Prom (T) Ltd akinywa dawa ya tambiko
Bosi wa kampuni ya mafuta ya Maurel et Prom (T) Ltd akipakwa dawa ya tambiko kwenye kipaji cha uso
Mabosi na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa katika tambiko hilo linalodaiwa kufanyika mapema wiki hii.
Za kitaa kutoka Mtwara zinadai kuwa bibi mmoja aliyeitisha Serikali kuwa ikifanya mchezo na haki za watu wa mkoa huo atabadili gesi kuwa maji, amewapigia tambiko Wafaransa wazungu wa Kampuni ya uchimbaji wa visima vya mafuta ya Maurel et Prom (T) Ltd yenye ofisi zake Chole Road, Msasani Peninsular, Dar es Salaam, baada ya kile kilichodaiwa drill yao ya kuchimbia mafuta kukatika mara tatu wakati wakichimba kisima cha urefu wa mita 3,000 chini ya bahari. Inadaiwa baada ya kuanza kuona maajabu katika kazi yao hiyo, fasta walijisalimisha kwa bibi huyo huko Mtwara na kukubali kufanyiwa tambiko ili mambo yanyooke, kama wanavyoonekana pichani hapo juu! Kama ni kweli, basi bibi anatisha! Lol!!.
JUX AMKANA VANESSA MDEE LIVE!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
PATA HABARI HARAKA ZITUFIKIAPO.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO
TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142
KARIBU TENA!
PICHA: Hisani ya Mtandao
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment