Staa wa muziki wa bongo fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' akilitawala jukwaa pamoja na baadhi ya wacheza shoo wake katika onyesho la kwanza la tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza lililofanyika mwishoni mwa wiki,tamasha hilo litaendelea kwenye miji mingine ya Bukoba na Kahama mwishoni mwa wiki..
Baada ya kazi ya kuwaburudisha mashabiki wake,Mara Wema Sepetu a.k.a shemeji nae akajiunga kumpa sapoti mpenzi wake jukwaani
Mmoja wa wasanii anaefanya vyema kwa sasa katika anga ya muziki wa bongofleva Vanessa Mdee a.k.a V Money akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mrindimo wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo,tamasha hilo limefanyika mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa wasanii anaefanya vyema kwa sasa kupitia wimbo wake mpya wa Ole Themba akiwa chini ya Kampuni mpya ya No Fake Zone,Linah Sanga akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mrindimo wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba lililofanyika mwishoni mwa wiki.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.















Hivi ndivyo wakazi wa Jiji la Mwanza walivyojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Msanii wa Bongofleva kutoka Mo Music akiimba jukwaani

Utulivu ulikuwepo wa kutosha ndani ya tamasha la Fiesta 2014 huku umati mkubwa ukishuhudia uzinduzi wa tamasha hilo jijini Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba,mwishoni mwa wiki.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Young De, akifanya vitu vyake ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba wakati wa tamasha la Serengeti fiesta 2014, lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.









0 comments:
Post a Comment